Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama hajasafiri na kikosi cha Simba SC, kilichoanza safari ya kuelekea mkoani Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma jiji FC.

Simba SC itakuwa mgeni wa mchezo huo wa Mzunguuko wa 21 utakaopigwa Jumapili (Januari 22), huku ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 47 katika msimamo wa Ligi hiyo.

Kikosi cha Simba SC kimesafiri kwa usafiri wa Anga (Ndege) kuelekea Mkoani Dodoma, lakini katika msafara wa kikosi hicho Chama hakuwepo, na hakuonekana kabisa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Hadi sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na Uongozi wa Simba SC, juu ya Kukosekana Kwa Mwamba huyo wa Lusaka.

Katika hatua nyingine Kiungo Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka nchini Ghana Augustine Okrah, amejumuishwa kwenye safari ya mkoani Dodoma.

Kiungo huyo hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kilichoikabili Mbeya City FC juzi Jumatano (Januari 18), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Wakati huo huo Wachezaji wawili wa Kimataifa waliosajiliwa klabuni hapo Ismail Sawadogo na Jean Baleke ni miongoni mwa wachezaji waliosafiri na kikosi cha Simba SC kuelekea Dodoma.

Rwanda yaituhumu DRC kwa kukiuka makubaliano
Mapambano vifo vya uzazi, watoto wachanga si ya Wizara pekee: Dkt. Batilda