Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chama ‘Mwamba wa Lusaka’ amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mzuunguuko wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi.

Chama ameshinda tuzo hiyo baada ya kuchagiza ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya As Vita Club ya DR Congo, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi (April 03) Chama alifunga mabao mawili na kutoa Assist moja na kuwashinda Ferjani Sassi wa Zamalek ya Misri, Amir Sayoud wa CR Belouizdad ya Algeria na Ricardo Goss wa Mamelodi Sundowns FC ya Afrika Kusini walioingia fainali.

Hi ni mara ya pili kwa klabu ya Simba kupata mchezaji bora wa wiki baada ya mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Msumbiji Luis Miquissone kuchaguliwa katika mzunguuko wa pili, baada ya mchezo dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly.

Simba SC inaongoza msimamo wa kundi A kwa kufiksha alama 13, na tayari imeshafuzu hatua ya Robo Fainali sambamba na mabingwa watetezi Al Ahly wenye alama 8 zinazowaweka kwenye nafasi ya pili, AS Vita Club wanashika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 4 huku Al Merrikh wakiburuza mkia kwa kumiliki alama 2.

Bumbuli: Hatujaridhishwa na adhabu ya Mwakalebela
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 7, 2021