Meneja wa klabu bingwa nchini England, Leicester City, Claudio Ranieri amekiri kuwa klabu yake haina ubavu wa kumzuia mshambuliaji Jamie Vardy kusaini kuichezea Arsenal.

Ranieri ameipa Arsenal matumaini ya kumalizana na Vardy aliopo nchini Ufaransa na kikosi cha England kinachoshiriki Euro 2016 kwa kudai kuwa mshambuliaji huyo ndiye mwenye kauli ya mwisho juu ya uhamisho huo.

Vardy ambaye alifanikiwa kufunga mabao 24 wakati Leicester ikiandika historia ya kutwaa taji la Premier League kwa mara ya kwanza msimu uliopita, anatarajiwa kufanya uamuzi wa kubaki King Power Stadium au kuhamia Emirates baada ya Euro 2016.

Claudio Ranieri akimpongeza Jamie Vardy baada ya moja ya michezo ya ligi kuu ya England msimu uliopita.

“Tunataka kumbakisha, lakini Arsenal wamesema watalipa fedha yote (pauni milioni 20) inayotakiwa kwa mujibu wa mkataba ili kuwaachia, lakini bado hajaridhia… Ni juu ya mchezaji kusema ndiyo au hapana,” alisema Ranieri akizungumza na Sky Italia.

Ranieri alisema ana matumaini kuwa anaweza kuwabakisha ‘mabingwa’ wake wote wakiwamo N’Golo Kante na Riyad Mahrez ambao pia wako mguu ndani mguu nje, na kuongeza mastaa wengine wanaowafukuzia kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi chao.

Video: Uwanja aliopigia push up Rais Magufuli umefikishwa Bungeni na Mbunge Bashungwa
Shomari Kapombe Ang'ara Zaidi Ya Wengine Azam FC