wafungwa 180 kutoka Gereza lenye Ulinzi mkali la Shimo la Tewa lililopo Mombasa wametolewa gerezani na kutakiwa kukamilisha vifungo vyao nyumbani

Kutolewa kwa wafungwa hao ni mkakati wa Mahakama na Polisi katika kupunguza msongamano uliopo gerezani ili kuepusha maambukizi ya virusi vya covid 19.

Imeelezwa kuwa idadi kubwa ya walioachiwa wametumikia robo tatu ya vifungo vyao na wametakiwa kumalizia adhabu zao nyumbani bila kufanya uhalifu wala makosa ya aina yoyote.

Wafungwa hao watakuwa chini ya uangalizi na watapangiwa kufanya kazi za kijamii chini ya uangalizi wa Polisi, na wametakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi katika vituo ambavyo walikamatwa ndani ya saa 48 baada ya kuachiwa.

Italia: Muuguzi aliyepata Corona ajiua
Miquissone apandisha bendera Msumbiji