Aliyekuwa mshambuiaji wa PSG, Wang Shuang anatarajia kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Wanawake China baada ya kuanza kufunguliwa taratibu kwa mji wa Wuhan ambao ndiyo kitovu cha maambukizi ya virusi Corona.

Kiungo huyo wa Wuhan Chedu Jiangda ni miongoni mwa baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho waliofungiwa katika mji huo kipindi ambacho kulikuwa na mlipuko mkubwa wa maambukizi ya virusi hivyo.

Kocha Mkuu Jia Xiuquan amethibitisha kuwa wachezaji wengine wa kikosi chake cha wachezaji 23, watajiunga baada ya April 08, 2020 ambapo mji wa Wuhan utafunguliwa rasmi.

China inajiandaa kucheza mchezo wa mtoano wa kufuzu kucheza michuano ya Olimpiki dhidi ya Korea Kusini, mchezo ambao utapangiwa tarehe nyingine baada ya kuahirishwa kwa michuano hiyo hadi mwaka 2021.

LIVE: Yanayojiri Bungeni leo
Mshtuko: afariki maduka yake mawili yakiteketea moto

Comments

comments