Sakata linaloendelea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) linazidi kuchuku sura mpya kila kukicha mara baada ya Maalim Seif kuibuka na kusema hakuna wa kumng’oa ndani ya Chama hicho.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa siku chache zilizopita Mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Prof. Ibrahim Lipumba alitangaza kumfukuza uanachama ndani ya chama hicho kitu ambacho si kweli.

Siku chache zilizopita, Prof. Lipumba alisema ameamua kumfukuza uanachama Maalim Seif  kwa kushindwa kazi na nafasi ya Katibu kumkaimisha Magdalena Sakaaya.

“Sijashindwa kazi, mimi ni Katibu Mkuu hadi nisimamishwe na Baraza Kuu, na yeye Lipumba kama ni Mwenyekiti alitakiwa lazima ahalalishwe na Baraza Kuu halali la Chama, tangu lini Katibu akapangiwa kazi na Mwenyekiti,”amesema Maalim.

Aidha, Maalim amesema kuwa Mahakama pekee ndio chombo kitakachoinuru CUF kutoka kwenye mgogoro huo.

Hata hivyo, Maalim ameitupa lawama zake kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), akidai kuwa kuna shinikizo kubwa la kumtaka Ofisa Mtendaji Mkuu kusajili wajumbe, ‘Feki’

Antoine Griezmann Amjaza Matumaini Jose Mourinho
Sintofahamu Ya Mali Yaichanganya TFF