Mwenyekiti wa Zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali ameibuka na kutamba kuwa kasi ya Emmanuel Okwi na John Bocco kuwa hakuna beki wa kuwazuia.

Amesema kuwa wachezaji hao wamekuwa chachu ya ushindi wa klabu ya Simba katika michuano ya ligi kuu msimu huu na kusema kuwa klabu hiyo itaendelea kufanya vizuri hata kwenye kombe la shirikisho Barani Afrika.

“Ukweli kasi ya Okwi na Bocco ni hatari hakuna beki wa kuwazuia na pia wamekuwa wanashirikiana na wenzao, hii ndio Simba ya siku zote,”amesema Dalali

Aidha, amesema kuwa ana imani kubwa na kasi hiyo itazidi kuongezeka kadri muda unavyozidi kwenda kwani wachezaji hao wamekuwa wanacheza kama mapacha.

Hata hivyo, Simba inatarajia kukwaana na timu ya Gendarmerie ya kutoka Djibout hapo kesho katika mchezo wa kombe la shirikisho Barani Afrika.

Video: Wabunge waogopa kukutwa ya Lissu, Watumishi wa umma kicheko
Msigwa aibua ufisadi mkubwa mradi wa uhamiaji mtandao (E-Immigration)

Comments

comments