Aliyekuwa beki wa Young Africans, Andrew Vicent ‘Dante’ amewakalia kooni viongozi wa klabu hiyo baada ya kuweka wazi kwamba bado kuna sehemu ya pesa zake za usajili anawadai.

Dante ambaye kwa sasa ni anaitukimia KMC FC, amesema sehemu fedha anazodai ni za usajili ammbazo ni shilingi milioni 32, ikiwa ni ya mkataba wa miaka miwili uliokuwa na thamani ya shilingi milioni 50.

Dante amesema awali alipewa sehemu ya pesa yake alipomaliza mkataba na kukaa chini na viongozi wa Young Africans ili kulipwa stahiki zake, ndipo alipokumbana na changamoto ya kutakiwa kukatwa baadhi ya fedha.

“Baada ya kumaliza mkataba na kwenda pale klabuni kwa ajili ya kujua tunaachanaje vizuri, ndipo waliniambia kwamba hela yangu inakatwa, nilipohoji walisema kuna vitu walikuwa hawakati ndio maana natakiwa nikatwe,”

“Nilihoji kwa nini haikuwa hivyo awali na kwanini hawakuniambia, basi sikuchukua kile ambacho walitaka kunipa na kwa sababu mimi najua pesa yangu ni nyingi kuliko kile ambacho wanataka kunipa mpaka sasa.” Amesema mchezaji huyo.

Beki huyo aliongeza kuwa tayari ameshaanza taratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba anapata stahiki zake zote zilizosalia kwenye klabu hiyo, yenye maskani yake makuu katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, jijini Dar es salaam.

Nchimbi asakwa Mwadui FC
PICHA: AMAVUBI watangulia CHAN