Mabingwa wa soka nchini Hispania Real Madrid wamefanikiwa kuipata saini ya beki wa pembeni kutoka nchini Austria na FC Bayern Munich David Alaba, ambaye rasmi ataanza kuonekana huko Estadio Santiago Bernabeu msimu ujao.

Alaba atakuwa mchezaji halali wa Real Madrid kuanzia Julai Mosi, kufuatia Real Madrid kushinda vita ya kumsajili dhidi ya klabu za England Manchester City, Chelsea na Liverpool.

Klabu nyingine iliyokua kwenye vita ya kumuwania beki huyo mwenye umri wa miaka 28, ni Mabingwa wa Soka nchini Italia Juventus FC, lakini mchezaji huyo inasemekana amezikacha klabu hizo na kukubali kujiunga na Real Madrid.

Real Madrid wamekamilisha usajili huo kwa haraka baada ya makubaliano kufikiwa na mchezaji, ambaye anaweza kujiunga na uhamisho wa bure na kupokea takribani Euro Milioni 80 kwa miaka minne kwenye mshahara wake.

Real Madrid ilianza kumfuatilia Alaba, baada ya mazungumzo ya beki huyo na uongozi wa FC Bayern Munich ya kusaini mkataba mpya kushindwa kupata muafaka.

Alaba ameitumia FC Bayern Munich katika michezo 408 huku akifunga mabao 32 na kutoa pasi 49zilizozaa mabao.

Amekuwa sehemu ya kikosi cha The Bavarians kilichotwaa mataji mataji 25 (Ligi ya Mabingwa Ulaya na Bundesliga Mara tisa).

Dudu baya mikononi mwa sheria
Trump aiombea heri serikali ya Biden