Baada ya kujaza uwanja wa Arena nchini Uingereza na kufikia rekodi waliovunja wasanii wakubwa nchini Marekani Davido atatumbuiza jukwaa moja na wasanii wakali wa dunia  Cardi B, Future Tory Lnez Migoes na wengine kwenye tamasha la Vest Villa  ambalo litafanyika nchini Ubelgiiji mwishoni mwa Februari 2019.

Davido ambae anafanya vizuri Afrika na dunia kwa ujumla, Januari 28, 2019 alishika nafasi ya pili kuujaza uwanja wa O2 London Mjini Uingereza baada ya Wizkid kushika nafasi ya kwanza kuvunja rekodi ya kuwa kijana mdogo barani Afrika kujaza uwanja huo.

Aidha Davido kupitia ukurasa wake wa instagram amepost picha na amegusia kuhusu tamasha hilo ambalo litawakilishwa na wasanii kibao na kuandika ujumbe huu “Festival season 2019….New level Unlocked” viwango vya juu vimefunguka.

Jina la msanii huyo linaendelea kushika kasi mara tu baada ya kuvunja rekodi mjini London huku akipata nafasi ya kushiriki kutumbuiza katika matamasha makubwa na wasanii wenye majina makubwa katika tasnia ya muziki duniani na kuipaisha vyema bendera ya Nigeria.

 

 

 

Serikali kuongeza nguvu sekta binafsi
Marekani yaishushia makombora Al-Shabaab

Comments

comments