Msanii mkongwe aliyekuwa mmoja kati waliounda kundi la Daz Nundaz, Daz Baba amefunguka kuhusu taarifa zinazosambaa mitaani na kwenye mitandao kuwa yeye ni mtumiaji wa dawa za kulevya na kwamba ndio chanzo cha kumpoteza kwenye muziki.

Daz Baba amekanusha taarifa hizo na kuwakosoa baadhi ya wadau wa muziki kwa kumtenga na kumchafua badala ya kumpa kazi kama msanii.

“Wananchafua vile halafu hamna lolote ambalo wananisaidia, kusema labda basi ‘huyu mtu labda tumpe show afanye tuone uwezo wake’, hapana… zaidi ni kunikandamiza nionekane mtu sio na riziki yangu ipotee,” Daz Baba aliiambia Ladha 3600 ya E-FM.

Msanii huyo alisema kuwa kwa muda mrefu amekuwa nyumbani kwao akiisimamia familia yake baada ya baba yake kuuawa, jambo ambalo amesema kuwa haliwezi kufanywa na ‘teja’.

Alisema amekuwa haonenaki sana katika maeneo mengi kama ilivyo kwa wasanii wengine kutokana na kutungiwa mambo ya kumvuruga zaidi.

Magufuli amruhusu Mbowe kufanya maandamano Hai
Video Mpya: Kazi Kazi - Profesa Jay Ft. Sholo Mwamba