Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amewatoa hofu wakazi wa kata za Mvuti na Msongole katika suala zima la usalama katika maeneo yao na kuongeza kuwa wataishi  huru bila ya hofu waliyonayo kwa sasa kufuatia mauaji na vitisho vinavyojitokeza kutoka wa baadhi ya wahalifu wachache wasiopenda  amani.

Mjema ameyasema hayo alipokuwa  katika muendelezo wa ziara zake  kwenye wilaya yake ya Ilala  kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, ambapo amekutana na wananchi  mbalimbali wa vijiji vilivyomo katika kata za Mvuti na Msongole na kusikiliza kero zao ikiwemo migogoro ya ardhi, matatizo ya miundo mbinu, hospitali, shule na suala zima la usalama.

Akijibu kero hizo na jinsi gani ya kuzitafutia ufumbuzi, Mjema amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa serikali ilikuweza kupata urahisi wa kutatua matatizo hayo ambayo kwa muda mrefu wamekuwa waki ya lalamikia, aliongeza kuwa serikali iko tayari muda wowote kusaidia wananchi na ipo kwaajili yao.

Kwa upande wa wananchi wa kata za Mvuti na Msongole wametoa kero mbalimbali na za muda mrefu ambazo zimekuwa ni tatizo kwao na kusema kuwa wana imani kwamba yeye atakuwa ndiye mwarobaini wa utatuzi wa migogoro hiyo ambayo imekuwa ni kiwazo cha maendeleo katika kata hizo.

”Tunakuomba utusaidie mkuu wetu wa wilaya kutatua haya matatizo ya miundo mbinu na migogoro ya ardhi, tunaehangaika sana hasa sisi wenye migogoro ya ardhi,tumedhurumiwa hatujui hatima yetu tutaenda wapi” Alisema mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Bakari.

Hata hivyo Mjema ametoa wiki moja kuhamishwa kwa wafanyakazi wa zahanati ya Mvuti waliokaa zaidi ya miaka thelathini  katika hospitali hiyo baada ya kupata malalamiko yanayowahusu watumishi hao  kutoka kwa wananchi, ”Natoa wiki moja kwa watumishi hawa wahamishwe katika hospitali hii ya Mvuti watafutiwe sehemu zingine za kufanyia kazi, kwani haiwezekani wakae muda wote huo sehemu moja.”alisema Mjema.

Kata za Mvuti na Msongole zimekuwa na matatizo mengi na ya muda mrefu hasa migogoro ya ardhi na uhaba wa huduma za kijmii kama Maji, Shule, Hospitali, Usafiri, Vituo vya polisi kutokuwepo hali ambayo inawafanya wananchi kuishi kwa hofu kufuatia kuwepo kwa mashamba poli mengi katika eneo hilo ambayo yamekuwa ni maficho ya wahalifu.

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kwa familia ya Dk. Masaburi
Mdee, Kubenea waanza kuonja joto la Mahakama kwa kumpiga Katibu Tawala