Diamond Platinumz amekamilisha alichowaahidi mashabiki wake leo kwa kuachia video mpya ya wimbo wake mpya wa ‘Fire’ aliomshirikisha Tiwa Savage wa Nigeria.

Video hiyo imejaa warimbwende mbalimbali wanaoonesha uzuri wao ndani ya mavazi ya kuvuta usikivu na macho ya kiume yanayopita mbele yao.

Kwa wale wachambuzi wa mavazi wanaweza kupata ‘assignment’ ya kuchambua mitindo mipya ya mavazi aliyotupia Dangote kwenye Fire iliyofunikwa na mazingira mazuri ya kutengenezwa studio.

Bila shaka video hii itaweka rekodi kubwa kwenye YouTube kwa kuangaliwa mara nyingi zaidi ndani ya muda mfupi.
Enjoy!

Magazeti ya Tanzania leo Juni 22, 2017
Video: Bavicha wawaka kukamatwa Meya wa Ubungo