Siku za nyuma kuna tetesi zilivuma kuhusiana na msanii Q-chief kusainishwa katika label ya WCB Wasafi iliyopo chini ya mwanamuziki Diamond. Diamond na Qchillah wapo mbioni  kufanya kolabo. Japokuwa  haijadhihirishwa wazi kuhusiana na swala la Qchillah kusainishwa WCB Wasafi.
Q-Chief amesema, “mimi nahisi project inayofuata Simba anahusika”.
Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amejipanga kumrudisha Q-Chief kwenye ramani ya muziki baada ya uongozi wake wa QS Mhonda kushindwa kufanya hivyo licha ya kudai kutumia zaidi ya shilingi milioni 200 bila kupata faida.
“Unajua lengo langu kama mimi au sisi vijana wa sasa hivi tunajaribu kuona tunavyoweza kufanya kazi kwa ushirikiano, so tuko na maongezi na bro tunaangalia tunawezaje kufanya kazi kwasababu ni mtu ambaye kwanza mimi namfeel halafu ambaye namuamini,” Diamond ameiambia Dizzim Online.
“Ni mtu ambaye najua kabisa yaani akibonyeza button hii basi huu mji mzima umechafuka. Kwahiyo siwezi kuyaongea mengi sema Watanzania watuombee dua tunachokiplan kifanyike vizuri,” ameongeza staa huyo.

Hivi karibuni muimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Abubakar Katwila amekuwa kwenye vita vya maneno na kampuni inayomsimamia ya QS Mhonda anayoishutumu kwa kushindwa kumfikisha popote licha ya uwekezaji mkubwa ilioufanya kwake.

Qchillah ameeleza kuwa anahisi QS Mhonda hakuwa tayari kufanya nae biashara kutokana na faida hewa aliyoipata baada ya kuingia mkataba nae, na kusisitiza kuwa Diamond ni mtu wa biashara hivyo kwa moyo mmoja yupo tayari kufanya nae biashara.

CAF Yaichimba Mkwara COSAFA
Marekani yasema Korea ya Kaskazini ni tatizo