Baada ya kuwatoa wasanii wake wa WCB na kuwa kimya kwa muda mrefu tangu alipoanchia ‘Utanipenda’, Diamond Platinumz amerudi tena na mzigo anaoumiliki akiwapa shavu mapacha wa Nigeria, P Square.

Mkali huyo wa Bongo Flava amewaweka mguu sawa mashabiki wake kupitia Instagram akiwataka wasiweka macho yao mbali na channel yake ya Youtube kwani ataachia audio/video ya wimbo wake mpya hivi punde katika channel hiyo.

“diamondplatnumzMy People!!!!!!!!! Subscribe to my Youtube Channel now so that you can be the first one to watch the HIT from SIMBA ft P-SQUARE!!!! (Najua unakiu kias gani….haya Jiunge na Channel yangu ya YOUTUBE sasa ili uwe mtu wa kwanza kushuhudia Mshine yangu Mpya Nilowashirikisha P-SQUARE! ) Cc @peterpsquare @rudeboypsquare #SimbaKaseMa,” ameandika Diamond.

Alshabaab yakiri kutekeleza shambulio la Kenya
Unyama: ISIS wamchinja msichana wa miaka minne kwa 'utani' aliofanya mama yake