Mshambuliaji wa Azam, Didier Kavumbagu aliyekuwa akiwindwa na Mbeya City amesaini mkataba na klabu ya Ligi Kuu ya Vietnam, Long An ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama Dong Tam Long An.

Kavumbagu anajiunga na timu hio kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliongezewa na Azam mwaka jana. Alijiunga na Azam akitokea Yanga baada ya kumalizika kwa msimu wa 2013/14.

Washambuliaji Souleymane Dibate kutoka Mali na Rafael kutoka Brazil ni wageni watakaompa Kavumbagu changamoto ya kupigania namba katika kikosi hicho cha Long An ambao ni mabingwa mara mbili wa Ligi ya Vietnam.

TFF Kuzungumza Na DRFA, KIFA
Yalivyoripoti Magazeti Ya Ulaya Kuhusu Usajili