Klabu ya Sunderland inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England, imevunja mkataba wa kiungo kutoka nchini Gabon Didier Ndong, baada ya kushindwa kujiunga na wachezaji wenzake tangu mwezi Julai mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo zimeeleza kuwa hadi wakati huu hakuna mawasilino yoyote na mchezaji huyo, na hawajui alipo. Hivyo, wameona njia rahisi ya kuachana nae ni kuvunja mkataba wake.

“Hatuna mawasiliano baina yetu, tumejitahidi kumtafuta ili tujue sababu zinazomfanya ashindwe kuwa sehemu ya timu tangu tukijiandaa na msimu mpya wa ligi daraja la kwanza lakini imeshindikana,” imeeleza taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo.

“Sunderland AFC itaendelea kuwa na haki za mchezaji huyo, licha ya mkataba wake kuvunjwa tutaendelea kufuatilia ili kurejesha gharama za klabu kupitia mkataba wake, ambao unatakia kulipiwa fidia,” alisema.

Hata hivyo, tayari klabu ya Sunderland ilikua imefikia makubaliano ya kumuuza Ndong kwenye klabu ya Torino ya Italia kwa ada ya Pauni milioni 6.6 mwezi Juni, lakini mpango huo ulishindikana baada ya mhusika kutoonekana. Mkataba wa Ndong ulikua unafikia kikomo mwaka 2021.

Hii sio mara ya kwanza uongozi wa klabu ya Sunderland kufikia hatua ya kuvunja makataba wa mchezaji, kwani waliwahi kufanya hivyo kwa beki kutoka Senegal, Papy Djilobodji baada ya kuonesha utovu wa nidhamu wa kushindwa kuripoti klabuni hapo kwa wakati.

Beki huyo aliigharimu klabu ya Sunderland kiasi cha Pauni milioni 8 mwaka 2016 wakati akihamishwa kutoka Chelsea.

Video: Prof. Lipumba adai yuko tayari kuachia ngazi
TCU yafuta vyuo lukuki

Comments

comments