Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa,  amefunguliwa milango ya kurejea Vicente Calderón Stadium yalipo makao makuu ya klabu ya Atletico Madrid, endapo ataona inafaa kufanya maamuzi hayo.

Milango kwa mshambuliaji huyo, imefunguliwa na meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone ambaye amekua akijitahidi kusaka mafanikio tangu alipokabidhiwa kikosi cha Los Rojiblancos mwaka 2011.

Simeone tayari amelipendekeza jina la mshambuliaji huyo kwa viongozi wa Atletico Madrid ikiwa ni sehemu ya kujipanga vyema kwa msimu ujao wa ligi kuu ya nchini Hispania pamoja na michuano ya barani Ulaya.

Meneja huyo kutoka nchini Argentina, amekiri kupendezwa na huduma ya Costa na anaamini kama atafanikiwa kurejea klabuni hapo kutakua na mabadiliko makubwa katika safu yake ya ushambuliaji.

Diego Costa alipokua akiitumikia klabu ya Atletico Madrid kabla ya kuhamia Chelsea mwaka 2014.

Hata hivyo taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la Daily Star la nchini England, zinaeleza kwamba Simeone, ameshinikiza kusajiliwa kwa Diego Costa kama silaha ya kuendelea kubaki Vicente Calderón Stadium kwa msimu ujao, na kama itashindikana atakua radhi kuondoka na kwenda kusaka changamoto mahala pengine.

Hata hivyo meneja mpya wa The Blues, Antonio Conte amesisitiza kutaka kufanya kazi na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, hatua ambayo huenda ikawa ngumu kwa viongozi wa Atletico Madrid kumrejesha Hispania.

Diego Costa aliuzwa na uongozi wa Atletico Madrid mwaka 2014 na kujiunga na Chelsea ya nchini England, lakini kiwango chake hakina makali kama ilivyokua Hispania.

Rais wa zamani wa Chad ahukumiwa ‘Kifungo cha maisha jela’
Zlatan Ibrahimovic Awachanganya Wadau Wa Soka Duniani

Comments

comments