Siku chache baada ya kuapishwa, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein ameanza kuunda serikali yake akianzia katika ngazi za juu za uongozi wa kitaifa.

Leo, Dk. Shein ametangaza kumteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa serikali hiyo. Kutokana na uteuzi huo, Balozi Seif anarudi katika nafasi hiyo aliyoitumikia katika Serikali ya Awamu iliyopita.

Haijafahamika nani atapewa nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais endapo itaundwa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo kikatiba inaweza kuwa imeota mbawa. Hata hivyo, uteuzi huo wa Dk. Shein unaonesha dalili za kuwepo kwa serikali ya umoja wa kitaifa ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais hutoka katika chama cha upinzani chenye wawakilishi wengi na kilichopata kura zisizopungua asilimia 10.

Hata hivyo, hakuna chama cha Upinzani kilichopata asilimia 10 za kura halali katika uchaguzi wa marudio, huku Chama Kikuu cha Upinzani, Chama Cha Wananchi (CUF) kikisusia uchagui huo.

Magufuli aongezewa orodha ya majipu
Mwanakwetu Agoma Kurejea Nyumbani