Hatimaye Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo imempitisha Dkt. Bashiru Ally kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Uamuzi huo umepitishwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Kikwete jijini Dar es Salaam kikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt. John Magufuli.

Dkt. Bashiru ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amechukua nafasi ya Komredi Abdulrahman Kinana aliyejiuzulu nafasi hiyo jana, hatua ambayo ilitengeneza mijadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Kabla kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Dkt. Bashiru alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kuchunguza mali za CCM akiteuliwa na Rais John Magufuli, kamati iliyowasilisha ripoti yake hivi karibuni. Ripoti hiyo inatajwa kuwa sehemu ya yatakayoatolewa maamuzi katika kikao hicho cha NEC-CCM.

 

Aliyeachiwa kwa muda gerezani afyatua risasi na kuua askari, raia
Askari ashtakiwa kwa kumuita mpinzani ‘Rais’ mtandaoni

Comments

comments