Waziri wa Maliasili na Utalii, na Mbunge wa Nzega Vijijini, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Dkt. Hamisi Kigwangalla, amechukua hatua za kisheria kwa wahariri na wamiliki wa gazeti la Jamhuri kwa madai kuwa wamekuwa wakimchafua katika machapisho yao.

Ambapo amechukua hatua ya kuwaandikia barua na amewataka wamuombe radhi kwenye machapisho mawili ya gazeti hilo yatakayotoka ukurasa wa mbele, na yawe yanafuatana au kutoa fidia ya shilingi milioni 500 kwa kuchapisha habari ambayo hawakuwa na uhakika nayo na akidai kuwa wamemchafua na kumzushia uongo.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na kampuni ya Uwakili ya FMD Legal Consultants &Advocates kwa Gazeti hilo amesema kuwa kwenye makala iliyotoka tarehe 12 – 18 Novemba 2019 waliandika makala yenye kichwa cha habari ‘WANASWA UHUJUMU UCHUMI’, ndani yake ilihusisha kampuni za Kitalii za Ker and Downey, chini ya makampuni ya Friedkin, na gazeti hilo lilimtaja Dkt. Kigwangalla kwa jina na kwa cheo kuwa anawalinda kampuni hii dhidi ya makosa yao ya kikodi.

Waraka huo wa madai, ambao umevuja kwenye mitandao ya kijamii, unasema kuwa gazeti hilo lilichapa habari hizo bila kuwa na uhakika nazo, wakijua ni za uongo na walifanya hivyo kwa makusudi kwa malengo ya kumchafua Dkt. Kigwangalla ambaye ni mtu mwenye heshima kubwa na mamlaka ndani ya jimbo lake, Chama Chake na nchi yote’

Na kwamba walisambaza sana kwenye mitandao ikiwemo ya kijamii bila hata kufanya uthibitisho wa habari zenyewe wala kumuuliza Dkt. Kigwangalla ambaye anatuhumiwa.

Hata hivyo waraka huu, ambao umewafikia gazeti la JAMHURI tarehe 6 January 2020, umekutana na gazeti lingine la JAMHURI la tarehe 7 January 2020, likiwa limemuandika tena Dkt. Kigwangalla.

 

 

TMA yatangaza ongezeko la joto Dar es salaam
Ndege yalipuka Iran na kuua abiria wote