Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali imeendelea kuwahakikishia askari wa jeshi la polisi, magereza na kitengo cha uhamiaji mazingira bora zaidi ya kazi na kuboresha maisha yao.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Dar24 hivi karibuni, Dkt Nchemba ametaja baadhi ya mambo yanayoendelea kukamilishwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za askari katika maeneo mbalimbali nchini.

“Tumeendelea kuboresha maeneo yao wanapokaa. Tuna nyumba ambazo ziko kwenye hatua za ukamilishwaji na hilo ni eneo ambalo limefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa. Sio tu kwa jeshi la polisi, magereza pale Ukonga ujenzi unaendelea na juzi Mheshimiwa Rais ametoa fedha nyingine kwa ajili ya kulipia nyumba za uhamiaji pale Dodoma,” Dkt Nchemba ameiambia Dar24.

Aliongeza kuwa Serikali pia imeendelea kuboresha vitendea kazi ikiwa ni pamoja na magari wanayotumia.

Amesema mbali na hayo, Serikali imeendelea kutia hamasa kwa jeshi hilo ili liwe na taswira kamili ya jeshi na sio taswira ya kiraia.

Angalia mahojiano yote hapa akingumzia pia hali ya msongamano magerezani na mkakati wa kupunguza wafungwa na mahabusu:

Chameleone awatimua kwa panga waombolezaji msiba wa Radio
Live Ikulu: Rais Magufuli akiwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa JWTZ