Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Dully Sykes ameponda uamuzi unaofanywa na baadhi ya wasanii kufanya video zao nje ya nchi kutafuta mazingira tofauti na ya ndani.

Dully ameiambia BBC kuwa wasanii wanaofanya maamuzi huo wana ulimbukeni wa kutaka kuwashangaza mashabiki wao kwa mazingira tofauti.

“Ni ulimbukeni,” alisema Dully. “Wanadhani watawashangaza watu kwa kuwaonesha mazingira mapya ambayo hawayajui,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Dully ambaye anatajwa kuwa mwanzilishi wa mtindo wa Bongo Flava iliyokuwa inaitwa ‘Mwanasesele’ alikumbushia jinsi alivyokuwa akikosolewa vikali na wasanii waliokuwa wanarap wakati huo.

Alisema wasanii kama J Mo na Mwana FA walifikia hatua ya kumchana kwenye wimbo wao wa ‘Ingekuwa Vipi/Ingekuwa Poa’, lakini leo Bongo Flava ndio muziki unaotamba zaidi.

Hivi sasa Dully anatamba na wimbo wake mpya wa ‘Inde’ aliomshirikisha Harmonize, video ikiwa imefanywa na

Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Gabon yazua mauaji
CUF yampisha Magufuli kufanya Mkutano Pemba