Sehemu ya familia ya Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, imeingilia kati machungu ya Mabingwa wa Italia kupoteza mchezo wa fainali wa kombe la Italia (Coppa Italia), kwa kufungwa na SSC Napoli Juzi Jumatano.

Juventus walikubali kuangukia pua katika mchezo huo kwa changamoto ya mikwaju Penati 4-2, na kumfanya Ronaldo Ronaldo kupoteza kwa mara ya kwanza fainali mfululizo katika maisha yake ya uchezaji soka la ushindani.

Kwanza alipoteza mchezo wa Super Cup na sasa hili linakuwa taji la pili mfululizo kwa Cristiano Ronaldo kulikosa ndani ya msimu mmoja jambo ambalo halijawahi kutokea.

Aliyeingia kati machungu ya Juventus ni dada wa Mshambuliaji huyo kutoka Ureno Elma Aveiro, ambapo amemshushia lawama kocha Maurizio Sarri kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, huku akimtetea ndugu yake.

Elma alimtetea kaka yake katika mitandao ya kijamii baada ya Sarri kusema Ronaldo na wachezaji wenzake walishindwa kutengeneza mashambulizi kwa haraka.

“Ni nini zaidi unaweza kufanya?  Mpenzi wangu (Ronaldo), huwezi kufanya miujiza mwenyewe. Nashindwa kuelewa kwanini unachezeshwa hivyo. Poa lakini, endelea kujituma,” aliandika Elma kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Sarri amekuwa akikosolewa kwa mtindo wake wa ufundishaji tangu alipofika katika timu hiyo na alikiri mwaka jana kwamba alihisi kama ametengenezwa kuwa gaidi wakati mwingine.

“Nilikuwa nikitafsiriwa kama Taliban kwa sababu kila wakati nilitaka kucheza mpira wangu, sasa haitoshi kwa sababu nimekuwa nikizisoma  tabia tofauti za wachezaji wangu.

Ikiwa ningelazimika kusikiliza au kusoma vitu ambavyo vinasemwa juu ya Juventus, ningekuwa chizi. Ninaendelea na kazi yangu tu.

Ningependa kuona timu thabiti zaidi na mitazamo fulani, lakini lazima tuzingatie tabia tofauti za wachezaji wetu,” alisema Sarri.

Young Africans yabisha hodi TFF
Jamie Carragher: Arsenal hawako vizuri