Rapa Eminem anatarajia kufanya utekaji wa nafasi za juu za mauzo ya albam mwaka huu atakapoachia albam yake mpya.

Mtandao wa HitsDailyDouble umeripoti kuwa Eminem ataachia albam yake ya tisa rasmi kutoka studio kabla ya mwaka huu kufikia ukingoni akikamilisha ahadi yake aliyoitoa mwaka uliopita. Albam hiyo inapikwa na Shady/Aftermath/Interscope.

Oktoba mwaka jana, Eminem alithibitisha kuwa anaandaa albam yake itakayoifuatia albam aliyoiachia mwaka 2013 aliyoibatiza ‘The Marshall Mathers LP’.

Baada ya kuachia ‘Campaign Speech’, Eminem aliandika kupitia Twitter, “msiwe na wasiwasi ninaandaa albam. Hiki ni kitu cha wakati huu tu.”

Kwa nguvu aliyonayo Eminem aingizapo mzigo sokoni, atakuwa na kazi ya ziada ya kuhakikisha anamfukuzia au hata kumpita Jay Z aliyefanya maangamizi ya mauzo ya albam yake ‘4:44’.

Simbu aing'arisha Tanzania mbio za marathon
Serikali yazungumzia taarifa za Gwajima kununua ndege binafsi