Mchekashaji nyota kutoka nchini Kenya Eric Omondi ametiwa mbaroni na jesho la polisi nchini humo, kufuatia kitendo cha kuliongoza kundi la vijana katika maandamano nje ya jengo la Bunge la nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za awali inadaiwa Omondi alikuwa akiliongoza kundi la vijana katika maandamano hayo kwa lengo la kupaza sauti wakiitaka serikali kuhakikisha inashusha gharama za maisha nchini humo.

Kutokana na maandamano hayo, inaelezwa kuwa sehemu kubwa ya biashara katika eneo linalozunguka Bunge, zililazika kusitishwa kwa muda kutokana na hofu ya usalama.

Ambapo inadaiwa kuwa polisi wamelazimika kuingilia kati maandamano hayo na kuwaamuru waandamanaji hao kutawanyika, bila mafanikio, jambo lililowalazimu kuwatawanya kwa kutumia vilipuzi vya kutoa machozi na kumkamata kiongozi wa maandamano hayo mchekeshaji Omondi na baadhi ya waandamanaji.

Kundi la vijana waandamanaji wakiongozwa na Eric Omondi

Katika maandamano hayo, kundi kubwa la vijana lilionekana kubeba mabango yaliyokuwa na jumbe mbali mbali zilizodhihirisha madai ya uhitajo wa unafuu wa gharama za maisha.

Hii si mara ya kwanza kwa Omondi kuanzisha maandamano na kuishia mikononi mwa jeshi la polisi, ikumbukwe mnamo Novemba 16, mwaka 2021 nyota huyo wa uchekeshaji alitiwa mbaroni baada ya kuanzisha maandamano ya vijana katika viunga vya Bunge la nchini hiyo.

Hanscana atoa somo zito kwa wasanii TZ

Watafiti KEMRI wagundua aina mpya ya Mbu mtata
Mpasuko kutengeneza Bahari mpya, Afrika kugawanyika