Rais wa klabu ya Inter Milan Erick Thohir, amesisitiza kuwa na imani kubwa na Frank de Boer ambaye juma hili amegubikwa na taarifa za kutimuliwa.

Thohir amevieleza vyombo vya habari mara baada ya mchezo wa ligi ya nchini Italia (Serie A) uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo ambapo Inter Milan walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Torino.

Kabla ya mchezo huo taarifa zilieleza kuwa, bodi ya wakurugenzi wa Inter Milan ilikuwa katika mpango wa kukutana mwishoni mwa juma hili, kwa lengo la kujadili mustakabali wa meneja huyo kutoka nchini Uholanzi.

“Tunataka kufikia malengo yetu, wote kwa pamoja tunamuamuzi Frank de Boer, kwa kazi yake anayoifanya, tumekutana mara kadhaa na tumeafikiana wazi kuwa meneja huyu bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kubaki na sisi.

“Tupo pamoja naye na vilevile tunatoa ushirikiano mkubwa kwa kila mmoja ambaye anahusika na kikosi chetu, ili tuweze kufanikisha malengo yaliopo.

“Mchezo wa soka una changamoto zake, kila mmoja anafahamu hilo, na kwa upande wa Inter Milan tunaamini tunapita katika njia ya kupanda na kushuka, lakini utafikia wakati mambo yatakaa sawa sawa.

“Ni muhimu sana kwa meneja na wachezaji wa Inter Milan kufanya kazi kwa pamoja, na kuelewa nini kinachohitajika ili kufikia lengo tunalolikusudia.

“Ni muhimu kupata matokeo mazuri. Na usiku huu tumeona jambo hilo limewezekana.” Thohir aliwaambia waandishi wa habari.

FA Yapanga Ratiba Ya Robo Fainali EFL CUP
Mourinho Ambwaga Guardiola, Man Utd Yatinga Robo Fainali