Dada wa Diamond Plainumz, Esma Platinumz amemshauri Hamisa Mobetto ambaye amezaa na kaka yake kuachana na sanaa ya muziki na kujikita zaidi katika biasahara ya mitindo kwa kile alichodai kuwa anafaa zaidi kufanya shughuli hizo kuliko muziki.

Amesema Hamisa anaimba kama yupo kwenye maombolezo na kusikitisha hivyo amemtaka afanye mazoezi zaidi kwani bado hayupo vizuri kwenye sanaa hiyo.

”Mi naona akae kwenye mitindo zaidi kwenye muziki naona bado” amesema Esma.

Hamissa Mobeto mwanamitindo ambaye ameamua kuingia katika sanaa ya muziki na hivi karibuni ameachia kibao chake kinachoenda kwa jina la ‘Madam Hero’ ni wimbo ambao uliwaibua watu wegi, wapo waliomsifia akiwemo Idris Sultan lakini pia wapo waliomponda.

Aidha Esma amezungumzia juu ya bifu yake na Hamisa Mobetto na kusema kuwa hana ugomvi wowote na mwanamitindo huyo.

” Mimi sina ugomvi na Hamisa, lakini  Hamisa akikosea mfano zile picha huwaga namsema, sipendagi kuishi na bifu halafu mimi na ishi mwenyewe navyotaka” amesema Esma.

Pia amezungumzia suala la mtoto wa Hamisa Dylan na kusema yeye na familia yake hawana tatizo na mtoto ndio maana amekuwa akimposti katika mitandao yake ya kijamii.

”Sisi hatuna tatizo lolote na mtoto, yule ni mtoto wetu damu yetu, hatuna tatizo naye ni watu tu wanajaribu kukuza vitu’ alimalizia Esma.

Sikiliza wimbo wa Hamisa Mobetto hapa chini toa maoni yako kama unaungana na Esma au unambariki mwanamitindo huyu kuendelea kutoa kazi nyingine za muziki.

Video: Bahati nzuri kwangu sijafa, bahati mbaya sana kwao sijafa- Tundu Lissu
Theresa May aahidi kufanya makubwa barani Afrika