Matarajio ya mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona ya  kumtumia mshambuliaji wao kutoka nchini Brazil Neymar kwenye mchezo dhidi ya Real Madrid (El Clasico), yameendelea kupata upinzani mkali, kufuatia rufaa yao ya kupinga adhabu ya mchezaji huyo kugonga mwamba.

FC Barcelona waliwasilisha rufaa ya kupinga adhabu ya kufungiwa michezo mitatu inayomkabili Neymar, baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano na kisha nyekundu, wakati wa mchezo wa ligi dhidi ya Malaga uliochezwa majuma mawili yaliyopita.

Taarifa iliyotolewa baadae na kamisaa wa mchezo huo, Jesus Gil Manzano, ilimbana zaidi Neymar baada ya kuonyesha kuwa, staa huyo wa zamani wa klabu ya Santos alimpigia makofi ya kejeli mwamuzi msaidizi huku akitoa maneno machafu wakati anatoka uwanjani na kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.Tukio hilo liliambatana na adhabu ya kukosa michezo miwili.

Uongozi wa klabu hiyo ya Camp Nou unajipanga kwenda kuisaka haki yao mbele ya mahakama ya usuluhishi ya masuala ya michezo (Court of Arbitration for Sport) leo Ijumaa, na ikiwa itashinda, Neymar ataruhusiwa kuivaa Real Madrid siku ya Jumapili huko Santiago Bernabeu.

Nandy awakana Dogo Janja na Bill Nas
Live: Kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge, Dkt. Elly Macha Dodoma