FC Barcelona wanaendelea kuhaha kufanya usajili ili kukiongezea nguvu kikosi chao kabla ya dirisha la usajili wakati wa majira ya kiangazi halijafungwa juma lijalo.

Wakati vita ya kumsaka kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Liverpool Philippe Coutinho ikiendelea,wababe hao wa Catalan wamejipanga kufanya usajili wa nyota watatu kutoka ligi ya nchini Ujerumani (Bundesliga).

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund  Ousmane Dembele, ni mmoja kati ya wanaowindwa huko Camp Nou, na tayari imeripotiwa mazungumzo kati ya viongozi wa pande hizo mbili yanaendelea kufanyika.

Wachezaji wengine kutoka ligi ya Ujerumani wanaowindwa na FC Barcelona ni kiungo wa Borussia Dortmund  Julian Weigl na Leon Goretzka wa Schalke 04. Wachezaji hawa wanatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya Euro milioni 40 kila mmoja.

Lakini imekua tofauti kwa Dembele ambaye amewekewa ngumu na viongozi wa BVB, hadi kiasi cha Euro milioni 150 kitakapotolewa kama ada yake ya uhamisho.

Video: LHRC wasema mahakama imepuuzwa, walaani kukamatwa Tundu Lissu
Juergen Klopp Kufanya Usajili