Chama cha soka nchini Italia (FIGC), kimethibitisha kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Antonio Conte, ataondoka mara baada ya fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka huu (Euro 2016).

Rais wa FIGC, Carlo Tavecchio amethibitisha taarifa hizo muda mchache uliopita kwa kusema, Conte, ambaye anafikiriwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea ya nchini England, amekubaliana na uongozi wake juu ya kuondoka mara baada ya fainali za mataifa ya barani Ulaya.

Tavecchio, amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kukaa chini na Conte na kupata muafaka wa jambo hilo, ambalo lilianza kuzungumzwa tangu mwezi uliopita kupitia vyombo vya habari hasa vya nchini England.

Amesema hawana kinyongo na Conte kuondoka mara baada ya Euro 2016, na daima wataendelea kuukumbuka mchango wake mkubwa ambao ameutoa katika timu ya taifa ya Italia tangu mwaka 2014.

Hata hivyo mkataba wa Conte, ulikua unafikia kikomo mwishoni mwa fainali za Euro 2016, na alikua anapewa nafasi kubwa ya kusainishwa mwingine mpya endapo angefikia malengo yanayokusuduiwa na viongozi wa FIGC.

BREAKING: Antonio Conte to step down as Italy coach after Euro…

BREAKING: Antonio Conte to step down as Italy coach after Euro 2016. More here: http://skysports.tv/tsrbOi

Publicado por Sky Sports em Terça, 15 de março de 2016

Mkurugenzi wa michezo wa Chelsea, Marina Granovskaia, ameripotiwa kuonekana mara kadhaa Italia, huku lengo kubwa la kuwepo nchini humo likitajwa kuwa ni kufanya makubaliano ya kuondoka kwa Antonio Conte.

Kwa sasa Chelsea, wananolewa na meneja wa muda Guus Hiddink, ambaye ataondoka mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea walianza kumsaka mbadala wa benchi lao la ufundi, mara baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho ambaye alionyesha kushindwa kuifanya kazi yake sawa sawa, kabla ya kutimuliwa mwishoni mwa mwaka 2015.

Magufuli: Vijana wasiofanya kazi walazimishwe, wapelekwe kambini
CUF wadai Serikali ni chanzo cha Maalim Seif kuishi Serena Hotel, wataja gharama ya chumba