Hatimaye jiji la Dar es Salaam litashuhudia ukomo wa foleni katika eneo marufu la Tazara, makutano ya barabara za Nelson Mandela na Nyerere kufikia Septemba mwaka huu.

Ukomo huo wa foleni katika eneo hilo utatokana na kumalizika kwa ujenzi wa barabara ya juu (flyovers) unaotarajiwa kumalizika Septemba mwaka huu ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya mwezi uliokuwa umepangwa kukamilika.

Kwa mujibu wa  Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, tayari ujenzi wa barabara hizo umefikia asilimia 88.82 na majaribio yataanza kufanyika Agosti mwaka huu.

“Nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa babarabara hizi, hadi sasa kila upande wa daraja umekamilika na kilichobaki ni eneo linaloshuka kwenye barabara,” alisema Prof. Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa alisema kuwa barabara hiyo ya juu ya Tazara haitakuwa pekee inayojengwa jijini Dar es Salaam na kutaja maeneo mengine ambayo mradi kama huo utatajwa kuwa ni eneo la Kurasini, Makutano ya Chang’ombe, Morocco na Mwenge.

Alisema kuwa Serikali imetenga kiasi cha sh. 20 bilioni katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2010/2019 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Mahakama yamshushia ‘mvua’ aliyewaua wazazi wake kwa shoka
Wapinzani walitaka Kanisa la KKKT kuigomea Serikali

Comments

comments