Mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ubunge wa jimbo la Monduli.

Taarifa za kujiondoa kwa Fred zimethibitishwa na Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa ambaye amesema uongozi wa chama hicho umekubali uamuzi wake.

Katibu huyo amesema kuwa uamuzi wa kumuondoa Fred ulitokana na maombi aliyoyawasilisha tena mwenyewe, licha ya kuwa alichukua fomu awali pamoja na makada wengine.

“Ni kweli nathibitisha ameomba kwa sasa sio wakati muafaka licha ya kuwa alionesha nia awali na wananchi wengi walimuunga mkono. Hivyo, chama kimekubali maombi yake na kimepitisha mgombea mwingine,” alisema Golugwa alisema jana.

Alieleza kuwa aliyeteuliwa kugombea katika uchaguzi huo mdogo wa marudio ni aliyekuwa diwani wa kata ya Lepurko, Yonas Masiaya Laizer.

Laizer atachuana kwenye uchaguzi huo na Julius Kalanga wa CCM ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema. Kalanga alijiuzulu na kuhamia CCM ambapo amepewa tena nafasi ya kutetea nafasi yake ya ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Mapadri wakumbwa na kashfa ya udhalilishaji wa kingono Marekani
Mkurugenzi ATCL akanusha Ndege ya Dreamliner kuwa na hitilafu