Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemtahadharisha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutovuka mstari dhidi ya Serikali katika mikutano yake ya hadhara.

Lema ambaye anaendelea na mikutano ya hiyo jimboni kwake amesikika akisema kuwa ataendelea kuzungumza ukweli bila kuogopa huku akiwarushia lawama wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya akidai kuwa wanafanya maamuzi kwa kufuata maagizo kutoka juu.

“Nimeteswa sana katika mji wa Arusha, lakini nawataka wafuasi wa Chadema msilipize kisasi kwa wanaohama chama. Leo wapinzani hawaruhusiwi kufanya siasa lakini Rais anazunguka nchi nzima,” alisema Lema na kumtaka mkuu wa mkoa huo kujipanga kikamilifu katika uchaguzi mdogo wa madiwani kuziba nafasi za madiwani wa Chadema waliojiuzulu akidai chama hicho kimejipanga kikamilifu.

Mwanafunzi akamatwa kwa kumkashifu Rais kwenye Facebook

Akijibu hoja hizo, Gambo alisisitiza kuwa atamshughulikia Lema kama atatumia mikutano anayoifanya kumtukana Rais na Serikali yake.

“Tumempa mbunge wa jimbo hili kibali cha kufanya mikutano na wananchi wake kwa sababu ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi. Hatuna sababu ya kumzuia. Lakini hatutakubali kusikia kwenye mikutano yake akimtukana Rais wetu na Serikali yake, akifanya hivyo tutamshughulikia,” Gambo anakaririwa.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wapinzani wamuache Rais atekeleze ahadi zake kwa wananchi kwani alipita nchi nzima wakati wa uchaguzi mkuu na kuwaahidi. Alionya kuwa watu wanaotaka kukwamisha ajenda za Serikali atawang’oa hata kwa greda.

Muasisi wa jina ‘Bongo Flava’ aanzisha kipindi cha historia ya Muziki huo
ACACIA yalipa mil.460 za ushuru, yanena mazito kuhusu makinikia