Mtangazaji maarufu na nguli, Gadner G. Habash amezungumzia faida na hasara anazoziona kwake baada ya kuachana na aliyekuwa mkewe, Lady Jay Dee.

Akiongea jana na kipindi cha Take One cha Clouds TV, Gardner alisema kuwa baada ya kuachana na mkewe na kuishi maisha ya nje ya ndoa ameweza kukutana na faida kadhaa pamoja na hasara lakini anafurahia zaidi maisha anayoyaishi sasa kwakuwa ndivyo aishivyo sasa.

Akitaja faida za kuwa ndani ya ndoa, Gardener alisema kuwa kwa kuwa ndani ya ndoa ni rahisi kuwa ‘committed’ na maisha na kujikita katika majukumu, “unakuwa responsible zaidi”.

Alisema kuwa ratiba ya maisha yako inakuwa na mipaka kwani wakati wote unahisi kuna mtu umemuacha nyumbani anahitaji uwepo wako, tofauti na sasa alipokuwa nje ya ndoa ambapo aligeuka kuwa mtu anayetembelea maeneo mengi (kuzurula) na kujikuta anatumia pia gharama kubwa katika ratiba hiyo mpya.

Alisema kuwa kwa uzoefu aliopata kwenye ndoa, chanzo kikubwa cha wanandoa kushindwa kudumu katika ndoa yao ni pale mmojawapo anapoanza kujifikiria yeye zaidi na kumsahau mtu mwingine.

“Mkianza kuwa mmoja anajifikiria yeye kwanza na kusahau mwenzake atajisikiaje, hapo ndipo mnaanza kubishana. Mkishaanza kubishana sana kila mmoja anaanza kupunguza upendo kwa mwenzake,” alisema Gardner.

Gardner ambaye anatarajia kuanza kusikika kupitia Jahazi ya Clouds Fm, April 11 mwaka huu alisema kuwa yeye na Lady Jay Dee hawana mawasiliano na kwamba mara ya mwisho walikutana wakati wanakamilisha taratibu za talaka yao.

Amesema hivi sasa yuko kwenye uhusiano na mwanamke ambaye hivi karibuni watu watamfahamu kwani huongozana naye kwenye matukio kadhaa anayohudhuria.

 

Magufuli aokoa shilingi bilioni 7.5 zinazotafunwa ‘kijanja’
Phil Thompson Ainyima Ushindi Liverpool Kama Itamtumia Sakho