Uongozi wa Chama Cha Soka Nchini England (FA), huenda ukakamilisha taratibu za kuthibitisha ajira ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo, baada ya kumfanyia usahili kocha wa muda Gareth Southgate.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa, Southgate anatarajia kutangazwa kuwa kocha kamili wa timu ya taifa ya England kwa makubaliano ya mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, ameonyesha kuwa na mustakabali mzuri wa kukiendesha vyema kikosi cha England, baada ya kupata matokeo ya kuridhishwa tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi kwa muda, baaada ya Sam Allardyce kutangaza kujiuzulu mwezi Septemba.

Muwakilishi wa Southgate amesema mazungumzo ya kimslahi kati ya FA na mteja wake yamefikia pazuri, na kuna dalili za kulipwa mshahara wa Pauni milioni 1.8 kwa mwaka.

Amesema huenda kiasi hicho cha mshahara kikaonekana kidogo katika jamii ya wanasoka nchini England tofauti na ilivyokua kwa Allardyce, ambaye alipaswa kulipwa mshahara wa pauni milioni 6.3 kwa miaka mitatu, lakini kwa upande wa Southgate ameonyesha kuridhishwa na kiwango hicho, na yupo tayari kusaini mkataba ndani ya juma hili.

Sergio Barila: Bacca Atabaki San Siro
West Ham Utd: Simone Zaza Halingani Na Thamani Yake