Takwimu kutoka tume ya uchaguzi nchini Liberia NEC zinaonyesha kuwa mwanasoka wa zamani George Opong Weah anaongoza katika matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu, akiwa mbele kwa majimbo 11 katia ya majimbo 15 japo kura zote hazijahesabiwa.

Mgombea anayefuatia ni makamu wa rais Joseph Boakai, ambaye anaongoza katika jimbo moja na mengine yanayosalia ameshika nafasi ya pili.

Mshindi katika kinyang’anyiro hicho analazimika kujipatia asilimia 50 ya kura zote ili aweze kutangazwa mshindi wa uraisi.

Iwapo itatokea kutopatika kwa mgombea atakayefikisha kiwango hicho uchaguzi wa marudio unapaswa kuwa mwezi Novemba.

Atakayetangazwa mshindi anachukua nafasi ya mwanamke wa kwanza Afrika kuwa rais Bi.Ellen Johnson Sirleaf anayemaliza muda wake kwa mjibu wa katiba ya taifa hilo na ambaye pia ni mshindi Nobel.

Kichuya aeleza mikakati yake
Video: CCM yashusha rungu zito, Ponda apewa siku tatu kujisalimisha Polisi

Comments

comments