Beki wa kati wa FC Barcelona Gerard Pique ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Hispania mara baada ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ambazo zitafanyika nchini Urusi.

Pique amekua na mahusiano mazuri na mashabiki wengi wa soka wa timu ya taifa ya Hispania kufuatia mchangom mkubwa alioutoa katika timu hiyo mpaka sasa, na huenda maamuzi hayo yakawashtua wengi.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 amesema anaamini itakapofika mwaka 2018, utakua ni muda mzuri kwake kukaa pembeni na kuwaachia wachezaji wengine wa taifa la Hispania kuendelea na majumu ya kulitetea taifa hilo kimataifa.

Amedai kuwa, kwa kipindi cha miaka saba alichoitumikia timu ya taifa ya Hispania, amepata mafanikiwa makubwa ya kutwaa ubingwa wa dunia pamoja na Ulaya huku akiwa sehemu ya wachezaji waliopita katika machungu makubwa ya kushindwa kutetea mataji hayo katika fainali za 2014 na 2016, jambo  ambalo amesisitiza hatolisahau maishani mwake.

Itakapofika mwaka 2018, Pique atakua amefikisha miaka 31 ya kuzaliwa, umri ambao bado ni mapema kwa mchezaji kama yeye kufikia maamuzi ya kustaafu soka la kimataifa.

Real Madrid Yaendelea Kupata Majanga
Ndugai afumua Kamati ya Bunge na kuisuka upya