Wanachama na mashabiki wa Young Africans, jana usiku walifika nyumbani kwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara na kukabidhi mchango wao kwa ajili aya matibabu.

Wanayanga hao waliongozwa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Jerry Muro na walimkabidhi Manara kiasi ya Shilingi milioni moja na elfu hamsini na tano (1,055,000) kama mchango wao.

Juma lililopita, Manara alianza kusumbuliwa na tatizo la jicho la kushoto ambalo limepunguza uwezo wa kuona. Hivyo anatarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu na safari yake huenda ikawa siku ya Jumamosi.

Wanayanga hao walichanga fedha hizo kupitia makundi mbalimbali ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

IMG-20160713-WA0025[1]IMG-20160713-WA0026[1]

“Nashukuru sana wenzangu, mchango huu mnaweza kuuona ni mdogo sana. Lakini ni mkubwa sana kwa kuwa gharama ni kubwa sana.

“Nyie sasa mredusha zile enzi za Yanga na Simba ambao walikuwa wakiishi undugu wa enzi zile. Msiba wa Yanga wanazika Simba, Yanga wanazika Simba.

Hivyo ni jambo zuri sana,” alisema Manara.

Rais Magufuli amsifu Meya na Wabunge wa Ukawa, wakutana na Dk Tulia
Magufuli awavaa JKT, Magereza, Zitto akosoa 'Mbunge' wake kutemwa na JPM