Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam limemkamata Mbunge wa Kawe, Halima Mdee nyumbani kwake kufuatia agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo alisema kuwa Mdee alikamatwa jana jioni akiwa nyumbani kwake Makongo Juu jijini humo, na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Oysterbay.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aliagiza kukamatwa kwa Mbunge huyo akieleza kuwa amemkashfu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Taarifa za kukamatwa kwa Mdee zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wilaya ya Kinondoni, Suzan Kaganda ambaye alieleza kuwa jeshi hilo limetekeleza amri ya mkuu wa wilaya.

Mbunge huyo machachari wa Chadema anaendelea kukumbwa na bundi la adhabu ikiwa ni siku chache zilizopita tangu alipopewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge kwa muda wa mwaka mmoja.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Amkejeli Trump, Adai Amemtumia Zawadi
Magazeti ya Tanzania leo Julai 5, 2017