Baada ya ‘kelele’ nyingi za mashabiki wa muziki wa kizazi kipya nchini kudai kuwa Harmonize amekuwa akimkopi karibu kila kitu Boss wake, Diamond Platinumz, msanii huyo ameamua kujibu mashambulizi

Kupitia Instagram, Harmonize ameonesha kukerwa na mfananisho huo na kutumia lugha zenye ukakasi kujitetea akidai labda kwenye video ya wimbo ujao avae ‘dera’ ili atofautishwe na Diamond.

Harmonize

Harmonize amepigiwa kelele zaidi za kumkopi Diamond hasa baada ya kusikika kwenye wimbo wa ‘Inde’ alioshirikishwa na Prince Dully Sykes.

 

Wimbo Mpya: Nay wa Mitego feat Tiki - Good Time
Waliovuliwa Uanachama Young Africans Wakimbilia TFF