Kiungo kutoka nchini rwanda na klabu ya Simba SC, Haruna Niyonzima ameshatua nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo kwenye mguu unaomsumbua na kumfanya asionekane uwanjani siku za karibuni kutokana na kuuguza majeraha hayo.

Siku kadhaa zilizopita Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara alisema Niyonzima atasafiri kwenda India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo kwenye mguu kutokana na maumivu yanayoendelea kumsumbua, ambapo alisema haitachukua zaidi ya wiki mbili atakuwa amerejea uwanjani kwa sababu ni upasuaji mdogo tu.

Niyonzima ambaye alisajiwa na Simba baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga amethibitisha kuwa yupo India na anatarajiwa kuanza matibabu muda wowote kuanzia sasa.

Niyonzima aliondoka nchini Tanzania, Jumanne ya Februari 20, mwaka huu kwa usafiri wa ndege ya Emirates akipitia Dubai kabla ya kuelekea nchini India.

Ikumbukwe kuwa Niyonzima hajaonekana uwanjani katika mechi kadhaa kwa takribani miezi mitatu sasa na imekuwa ikielezwa kwamba ni kutokana na kuwa majeruhi.

Kimenuka Kagera Sugar, Mexime atoa tamko
Serikali yafuta ada mpya kwenye riadha

Comments

comments