Kiungo Mshambulaiji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Hassan Dilunga ‘HD’ amesema mchezo wa Jumamosi dhidi ya Young Africans wanauchukulia wa kawaida kama ilivyowahi kusemwa mapema msimu huu.

Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara aliwahi kutangaza hadharani kuwa, Simba SC sio kipimo cha Dabi katika soka la Tanzania, na sasa inaaminika kipimo cha klabu anayoitumikia ni Azam FC.

HD amejitosa kuuzungumzia mchezo huo ambao Simba SC watakua wenyeji uwanja wa Benjamin Mkapa, baada ya kikosi chao kurejea nchini jana Jumanne (Desemba 07) mjira ya usiku kikitokea Lusaka-Zambia.

Mchezaji huyo anaamini maneno yaliyowahi kusema na Msemaji wa Young Africans yanapaswa kuheshimiwa kutokana na kutambua Simba SC sio kipimo cha Dabi kwa upande wa klabu hiyo ya Jangwani.

HD amesema kikosi chao kinaendelea kujiandaa kuelekea mchezo huo kama ilivyowahi kuwa kwenye maandalizi ya michezo mingine, na hawaupi uzito mchezo huo kama mchezo wa Dabi.

“Derby imeshabadilishwa. Tuliambiwa Derby ni Azam FC na Yanga, hivyo sisi tunakwenda kucheza mechi ya kawaida ya ligi kama zilivyo mechi nyingine” amesema HD

Mshindi wa mchezo wa Jumamosi atapata nafasi ya kuongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa nafasi, tofauti na sasa ambapo wawili hao wamepishana kwa tofauti ya alama mbili.

Young Africans inaongioza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 19, huku Mabingwa watetezi Simba SC wakishika nafasi ya pili kwa kufikisha alama 17 baada ya kila mmoja kucheza michezo saba.

Oscar Oscar: Inasikitisha kwa kweli
Nick Cannon amwaga machozi kifo cha mtoto wake mchanga