Hali ya hatari imebainika  katika kitengo cha afya cha hospitali ya Gauteng nchini Afrika Kusini, baada ya kamati maalum ilyoundwa kufanya uchunguzi katika hospitali hiyo kubaini kuwa watu ambao hawana taaluma ya udaktari hushiriki kufanya upasuaji wa kuchunguza miili ya marehemu (Postmortem).

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Afrika Kusini, kamati hiyo maalum iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Mary Ann Dunjwa, imeeleza kuwa baadhi ya watu wanaoshirikia upasuaji na uchunguzi wa miili ya marehemu ni madereva na wafanya usafi wa hospitali hiyo.

“Kamati ya kitengo cha taifa cha afya imeainisha kuwa kuna watu hao ambao hawana utaalam wala mafunzo, kwahiyo ni dhahiri kuwa wamekuwa wakifanya kazi hiyo [ya upasuaji na uchunguzi wa maiti],” Dunjwa anakaririwa na News24 ya Afrika Kusini.

Taarifa ya kamati hiyo ilitolewa wakati mkurugenzi mkuu wa Kitengo cha Taifa, Malebona Precious Matsoso alipokuwa akizungumza na kamati hiyo kuhusu mgomo uliokuwa unaendelea wa wafanyakazi wa hospitali hiyo ya Gauteng.

Awali, kitengo cha afya cha Gauteng kilikanusha taarifa hizo kikidai kuwa watu hao hawahusiki kufanya uchunguzi wa miili ya marehemu bali huwasaidia madaktari wenye taaluma husika kufanya maandalizi ya kazi hiyo.

Chanzo cha kifo cha rapa Prodigy wa Mobb Deep chawekwa wazi
Florian Lejeune Kuikamua Newcastle Utd £8.7