Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amesikitishwa sana na matukio yanayofanywa na polisi ya kuumiza raia huku jukumu lao likiwa ni kulinda wananchi wake, Heche amekumbushia tukio la kijana alieuawa Mbeya, tukio la mdogo wake kusababishiwa ulemavu na tukio la Mwanza la mama mmoja kupoteza kichanga chake akiwa mikononi mwa polisi.

Ameshangazwa ni kwa vipi mtu anaweza kuuwawa na polisi kwa kuchomwa kisu mgongoni tena akiwa amefungwa pingu, amedai kuwa kwa kufanya hivyo muuaji alikuwa amedhamiria kwa kile alichokuwa anakifanya kwani mjeruhiwa hakuwa anapambana.

”Nilijua mikononi mwa polisi ni sehemu salama, wiki mbili zilizopita kijana Allen alikufa katika mazingira tata kule Mbeya, Mwanza mama aliyekamatwa na kunyimwa dhamana mtoto wake mchanga alikufa. Leo ni kwangu mdogo wangu ameuwawa kikatili sana mikononi mwa polisi. Maisha yangu yote nimeyatoa kupigania haki ili watu wasionewe, mtuhumiwa asifanywe mkosaji na kuhukumiwa kabla ya vyombo vya sheria kumhukumu,”  Heche.

Ameongeza ” Mwaka jana mdogo wangu mwingine aliumizwa vibaya sana na polisi. IGP Mangu na RPC waliokuwa Tarime walilipa uzito suala hilo lakini walipoondolewa, suala liligeuzwa kisiasa na wale vijana waliokua wamemjeruhi mdogo wangu ambaye mpaka sasa sikio moja halisikii,wakarudishwa kazini kinyemera na kuhamishwa Tarime kama kunikomoa. Mimi nimewahi kutishiwa kuuwawa kituo cha polisi, najisikia maumivu makubwa mno lazima Watanzania wakatae hali hii”.

Aidha Heche amesema  wakati muafaka ukifika atazungumza swala hilo kwani watu wanakufa na kuumizwa mikononi mwa polisi bila matukio kujulikana wala kutangazwa na kuweka wazi.

Mikataba ya Kanumba, Mzee Majuto mikononi mwa Mwakyembe
Basi lapata ajali mkoani Kagera

Comments

comments