Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amefikishwa mahakamani na kupelekwa mahabusu ndogo akisubiri kujibu kesi inayomkabili mara baada ya wakili Nchimbi kuiomba mahakama kumjumuishwa kwenye kesi inayowakabili vigogo saba wa chadema kesi ya uchochezi na kuhamasisha maandamano.

Heche amefikishwa mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu leo, Aprili 5, 2018.

Hata hivyo mbali na Heche kuna wafuasi wengine zaidi ya 20 wa Chadema wanashikiliwa na polisi kanda Maalumu wakiwa wanasubiri jalada kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP, ili kujua hukumu yao.

Ambapo wafuasi hao walikamatwa Aprili 3, mwaka huu.’

”Tunasubiri jalada kutoka kwa DPP ili kujua kama watafikishwa mahakamani au watapewa dhamana ya polisi” amesema Wakili Kihwelo.

Aidha ameongezea kuwa endapo ikashindikana kwa siku ya leo kufikishwa mahakamani au kupewa dhamana watawasilisha maombi yao Makahakama kuu.

 

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 12
Muigizaji Salman Khan atupwa jela miaka mitano

Comments

comments