Uongozi wa klabu ya Young Africans umetoa kauli kuhusu mustakabali wa Kocha Mkuu wa klabu hiyo Cedrick Kaze, baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Coastal Union, Jana Alhamis (Machi 04) jijini Tanga.

Kaze alionja uchungu wa kupoteza mchezo katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza, tangu alipokabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi cha klabu hiyo mwishoni mwa mwaka 2020.

Uongozi wa Young Africans kupitia Kamati ya Mashindano umetoa kauli ya kuendelea kuwa na imani na kocha huyo kutoka nchini Burundi.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Injinia Hersi Said imeeleza kuwa, Kocha Kaze alijiriwa klabuni hapo kwa mipango ya muda mrefu, hivyo wataendelea kuwa naye, huku wakiamini ipo siku atarejesha heshima ndani ya Young Africans.

 ”Tulimleta Kaze kwa ajili ya mpango wa muda mrefu, hivyo hatufikirii kuachana nae kwa sasa, Niwatake wanayanga mashabiki na wanachama wasikubali kuingizwa kwenye mijadala ambayo inalenga kutuvuruga,”

“Viongozi na wadhamini kila mmoja anaimani kubwa na mwalimu kaze,”

“Wakati mwingine kuna Mambo yanatokea nje ya uwezo wake lkn hiyo haiwi sababu ya kuona hawezi kutufikisha tulikokusudia,kuna watu wengi wanatumika vibaya kwa lengo la kutunyima utulivu na kutugawa hasa katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye mafanikio ya malengo yetu makuu,kuwa na timu Imara za vijana,wadada,na timu ya wakubwa pia kuelekea kwenye mfumo mpya wa uendeahaji club.”

“Ni vema sana wanayanga kajiepusha na hiyo mijadala na badala yake mkajikita katka kuisaport club yetu ktk nyanja zote,kwani malengo yetu bado ni yaleyale kuchukua ubingwa na kombe na FA.”

“Daima mbele nyuma mwiko.” Imeeleza taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.

Kigonya aitwa The Cranes
Mvua yamnyeshea Mahmoud Kahraba