Mwanamuzi nguli wa bongo fleva Ruta Maximilian maarufu Bushoke afunguka sababu za ukimya wake kwa kipindi kirefu bila kutoa wimbo licha ya kuwa sehemu kubwa ya mashabiki wake wakiwa na shauku ya kuhitaji kumsikia na kumuona akiwa katika mzunguko wa muziki kama ilivyokuwa kwa wasanii wengine.

Amesema kuwa kwa kipindi kirefu amewekeza nguvu na akili yake kwenye upande wa muziki wa ‘Live band’, na kwamba ndio kitu pekee ambacho amekuwa akikifanya kwa kipindi chote, tangu alipositisha kuachia nyimbo redioni na kwenye patforms mbali mbali.

Bushoke ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na Dar24 Media muda mfupi baada ya kumaliza kutumbuiza kwenye onyesho la ‘Cheers 2023’ mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es salaam.

Aidha mwimbaji huyo nguli aliyewahi kutamba na vibao kama ‘Mume bwege’, ‘Dunia njia’, ‘Usiende’ na nyingine nyingi, ameweka wazi kuwa haikuwa rahisi kwa yeye kufanya uamuzi wa kuhamia kufanya muziki wa live band, na kusalia kutumbuiza kwenye mahoteli na kumbi mbali mbali za starehe, lakini ilimlazimu kufanya hivyo, kutokana na uhitaji mkubwa wa kujaribu uzoefu mpya nje ya alichokuwa akikifanya hapo awali.

Bushoke. Photo/Unknown

“Muziki wa Live Band unamanufaa, lakini sio pesa, niliwahi kujiuliza nahitaji umaarufu wa kubakia naimba tu, au nataka kuimba muziki ambao inabidi pia nijifunze zaidi?, kwa maana kujulikana mwanamuziki sio kuwa mwanamuziki, kwa hivyo mimi nilichunguza vyote viwili na nikasema nifuate hiki cha Live Band, na nilipiga hesabu nikakiona hakina hela lakini kina manufaa mengine.” amesema Bushoke.

Kwa hiyo muziki basi tena..?

Licha ya hayo, nyota huyo ameeleza mikakati aliyonayo kwa mwaka mpya wa 2023, ikiwamo mpango wake wa kuachia nyimbo kadhaa ili kuhakikisha anakata kiu ya mshabiki wake.

“Ninachoweza kusema watu wasubiri kazi, na ninajua kwamba wamesubiri sana, lakini nawaambia sasa hivi hawatasubiri sana muda si mrefu nitawapatia kitu roho inapenda, nitajitahidi kutoa kitu kizuri cha kisasa naimani watafurahi” ameongeza.

Also read: ‘FOA’ ya Diamond album bora ya mwaka AEAUSA

Upelelezi kesi ya mmliki Cambiasso na wenzake watano wakamilika
TRA yavunja rekodi 2022