Tabia ya ulawiti na mapenzi ya jinsia moja karne hii imetawala kwa kasi sana kiasi ambacho inajenga hofu kwa wazazi wenye watoto hasa wale wanaosoma katika shule za jinsia moja za bweni.

Ambapo hofu kubwa imetawala kwa wazazi na walezi wa kata ya Igogo mkoani Mwanza kufuatia kuzuka kwa tabia za baadhi ya wavulana wanaodaiwa kutoroka shule na kwenda mapangoni kujihusisha na vitendo vya ngono za jinsia moja na kuingiliana kwa zamu kinyume na maumbile yao na kinyuma na maadili.

”Ulawiti upo na wanaridhishana ukiangalia mtoto ukimuuliza anakwambia alianza vipi utakuta ni chain ndefu amefundishwa na yeye anazichukua zile tabia anazipeleka mashuleni” amesema kiongozi wa kata ya Igogo.

Amesema Wanafunzi baada ya kwenda shule hujificha kwenye mapango 7 yaliyo karibu na shule na kulawitiana kinyume na maadili.

Zaidi ya watoto 20 kuanzia umri wa miaka 11 hadi 22 wanatajwa kujihusisha na vitendo hivyo vya kuingiliana wenyewe kwa wenyewe huku wengine wakiingiliwa na watu waliowazidi umri.

”Nilikuwa nacheza mtu akaja  akaniita nikakataa akanikamata na kunibaka amesema kijana mwenye miaka 12 aliyelawitiwa na mtu asiyemfahamu katika kata hiyo.

Aidha wakazi wa kata hiyo wameiomba serikali iwasaidie kukomesha vitendo hivyo wakishirikiana na wazazi wenyewe kwani wazazi huwalea watoto wao si waharibike bali waje kuwa tegemezi hapo baadae.

Wazazi wanapaswa kuwa makini sana kwani vitendo hivi vipo sana karibu maeneo yote siyo mjini sio vijijini watoto wapewe elimu juu ya kukabiliana na watu wenye tabia hizo na kuhimizwa kutoa taarifa mapema pindi wakiona mtu wa namna hiyo, pia waambiwe madhara ya tabia hiyo kwani inawezekana wakawa wanafanya wasijuwe hasara zake.

Bilionea Dkt. Shika sasa kuwanyoosha, mabilioni yatua nchini
Lusekelo: Nampenda Diamond, simpendi Alikiba