Aliyekuwa waziri wa Sheria na Masuala ya Kikatiba nchini Martha Karua ameibuka kuwa mgombea mwenza bora zaidi wa Raila Odinga kabla ya tarehe ya mwisho ya Mei 16 kwa wagombea urais kuwasilisha majina hayo kwa tume ya uchaguzi ambapo Mgombea urais wa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga hatimaye amemteuwa kiongozi huyo wa Narc-Kenya kuwa mgombea mwenza.

Akimtaja kwenye hafla iliyofanyika nje ya Jumba la Kimataifa la Mikutano (KICC) Raila alisema kwamba Jopo la Azimio la Kuteuwa Mgombea Mwenza lilitoa ripoti na kusema Karua aliibuka bora kwa nafasi hiyo.

Kiongozi wa Narc-Kenya Martha Karua katika mkutano wa Azimio uliofanyika Jumapili, Mei 15, Kamukunji, Nairobi.

Kiongozi wa Narc-Kenya Martha Karua ambaye mchango wake katika siasa za Kenya ni mkubwa sana ni mkongwe wa vuguvugu la kutetea demokrasia nchini Kenya miaka ya 1990 na kiongozi wa Narc Kenya, anaripotiwa kushika nafasi ya juu zaidi katika orodha fupi ya watu watatu waliopendekezwa kuwania nafasi ya mgombea mwenza wa Raila na jopo aliloteua kuwahoji watarajiwa.

Pia aliorodheshwa bora kuwashinda makamu wa rais wa zamani Kalonzo Musyoka na Peter Kenneth, mbunge wa zamani na majina mengine kwenye orodha ya walioteuliwa katika jopo la uteuzi katika viwango vya kuidhinishwa kwa nafasi hiyo, kulingana na matokeo ya kura ya maoni ya Aprili iliyoidhinishwa katika The EastAfrican.

Jopo hilo liliwahoji magavana Charity Ngilu (Kitui), Hassan Joho (Mombasa), Lee Kinyanjui (Nakuru) na Wycliffe Oparanya (Kakamega) kwa nafasi ya mgombea mwenza wiki iliyopita.

Wengine walikuwa ni Mwakilishi wa Kike wa Murang’a Sabina Chege, Waziri wa Kilimo Peter Munya na aliyekuwa mbunge wa Emgwen Stephen Tarus.

Jopo hilo lilikuwa likiwakagua wagombea hao kwa kuzingatia sifa za kikatiba, uelewa wa serikali, haiba, weledi wa kisiasa, utangamano na uaminifu kwa mgombea urais wa Azimio.

Hata hivyo Raila, kiongozi wa upinzani ambaye anawania urais kwa mara ya tano katika uchaguzi wa Agosti 9 akiungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta, ndiye aliyeamua mwisho kuhusu nani atakuwa mgombea mwenza katika muungano wake wa Azimio One Kenya na kumfanya Karua kuwa miongoni mwa Wanawake Viongozi wa juu wa serikali katika Afrika Mashariki endapo Raila atapita katika kiti hicho cha Urais.

Kwa upande mwingine Naibu Rais William Ruto, mshiriki mwingine aliye mbele katika kinyang’anyiro cha kumrithi Rais Kenyatta, pia anaaminika kuwa wakati fulani aliwazia kuhusu kumchagua mgombea mwenza wa kike.

Kuongezeka kwa kimo cha Karua katika muungano wa Odinga kumezua gumzo hasa katika vuguvugu la kutetea haki za wanawake nchini Kenya, ambalo limeongeza ushawishi wake kwa wagombea wakuu wa urais kuchagua wagombea wenza wa kike.

Mnamo Alhamisi, alikuwa kivutio kikubwa katika hafla ya kusherehekea miaka 70 ya Shirika la Maendeleo ya Wanawake, shirika mwavuli la vikundi vya ustawi wa wanawake mashinani, mjini Kisumu.

Tume ya uchaguzi, chini ya shinikizo kutoka kwa watetezi wa haki za wanawake, hivi karibuni ilikataa orodha ya watu waliopendekezwa na vyama vya siasa kwa viti maalum kama vile vijana, wanawake na watu wanaoishi na ulemavu kwa kutofuata sheria ya theluthi mbili ya jinsia.

Vyama vya kisiasa pia viliweka mazingira mazuri ya usawa wa kijinsia katika bunge lijalo kwa kutoa uteuzi wa moja kwa moja kwa wagombea wa kike waliochaguliwa katika ngome zao katika kura za mchujo za hivi majuzi, na hivyo kuongeza nafasi zao za kushinda.

ASFC: Simba SC Vs Young Africans kupigwa CCM Kirumba
Young Africans yaitangazia vita Mbeya Kwanza FC